Overblog
Edit post Follow this blog Administration + Create my blog
HABARI ZA UHAKIKA

MWINYI KAZIMOTO AMPA KIPONDO MUANDISHI WA HABARI

February 11 2016 , Written by raphael Published on #michezo

Kiungo mkongwe wa Simba, Mwinyi Kazimoto anatuhumiwa kumpiga mwandishi wa habari, hali iliyosababisha afikishwe katika kituo kikuu cha Polisi cha Shinyanga.

Kazimoto amefikishwa katika kituo hicho kilicho karibu kabisa na hospitali ya mkoa wa Shinyanga kwa madai ya kumshambulia mwandishi wa gazeti la Mwanaspoti, Mwanahiba Richard.

Imeelezwa, Kazimoto alimshambulia Mwanahiba baada ya mazoezi ya Simba yaliyofanyika katika Uwanja wa Kambarage uliopo katika eneo la Majengo mjini Shinyanga.

Mara baada ya mazoezi, inadaiwa Kazimoto alimvamia Mwanahiba na kumpiga akidai aliandika stori kwamba kiwango chake pamoja na wachezaji wengine katika mechi mbili za Simba dhidi ya Mbeya City na Tanaznia Prisons hakikuwa kizuri na wanapaswa kuchunguzwa.Kazimoto alionekana kutofurahishwa na habari hiyo iliyoonekana ni kama tuhuma, hivyo kupandwa na hasira hadi kuingia katika mgogoro huo na Mwanahiba.

Inadaiwa baada ya kipigo hicho, Mwanahiba aliripoti katika kituo hicho cha polisi na kupewa hati ya mashitaka (RB) yenye yenye namba SHY/RB/895/2016, fomu ya matibabu (PF3) kisha akapelekwa hospitali kwa matibabu.

Kazimoto hakupatikana kulizungumzia suala hilo, pia hakuna kiongozi wa Simba aliyelizungumzia, huku kukiwa na hekaheka ya kutaka kulimaliza kwa amani jambo ambalo linaonekana kupingwa na upande wa wanaolalamika.




MWANAHIBA RICHARD


Kwa upande wake Mwanahiba, alisema aliandika stori iliyokuwa ikieleza viongozi wa Simba kutoridhishwa na baadhi ya wachezaji wa Simba akiwemo Kazimoto baada ya wao kupoteza mchezo kwa kufungwa na Prisons kwa bao 1-0 mjini Mbeya katika mzunguko wa kwanza wa Ligi Kuu Bara.

“Ilikuwa ni stori ya mwaka jana, leo Kazimoto akaniita na kuanza kuniuliza akitaka nimwambie kiongozi gani aliyeniambia. Nikamueleza si kazi yake, kifupi niliandika na anajua kama hilo lilitokea.

“Alipoona nimemzidi hoja, akaanza kunishambulia kwa ngumi na mateke. Akanipiga hadi aliponiumiza kichwani, wakati huo wenzake walikuwa kwenye basi wanashuhudia, ndiyo Mgosi akawahi kushuka na kuniokoa,” alisema Mwanahiba.

Lakini Mhariri wa Mwanaspoti, Michael Momburi amesema suala hilo linashughulikiwa.

“Kweli hilo suala lipo, limefikishwa polisi na sisi tunaendelea kufuatilia. Hakika si suala sahihi na halifurahishi na tayari tumelikabidhi suala hilo kwa mwanasheria wa kampuni analishughulikia kwa kushirikiana na RPC wa Shinyanga,” alisema Momburi.
Chanzo: salehjembe.blogspot.com

Share this post
Repost0
To be informed of the latest articles, subscribe:
Comment on this post